Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(Nyaumata Mkoani)

Vitengo

kitengo

Majukumu

Kitengo cha tiba na matunzo (CTC)

 Huduma zinazotolewa ni upimaji wa maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI,

Kuanzisha kwa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI, ushauri na nasaha na  matibabu ya magonjwa nyemelezi.

Famasi

Kitengo hiki kinahakikisha  upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na  vifaa vya uchunguzi na matibabu.

Kitengo cha mionzi

kitengo hiki kinahakikisha utoaji wa huduma za X-ray na Ultrasound

Kitengo cha Maabara

Kutoa huduma za maabara kwa utambuzi wa magonjwa, upimaji na utoaji wa ushauri wa kitaalam ili kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa mgonjwa

Kitengo cha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa

Kushughulika na usajili wa mgonjwa, kutunza kumbukumbu  za mgonjwa, uainishaji wa takwimu za kitabibu

Kitengo cha fedha

Hushughulika na usimamizi wa fedha na ripoti zinazohusiana na fedha

Kitengo cha manunuzi

Hushughulika na manunuzi yote yanayofanyika Hospitalini.

Kitengo cha TEHAMA

Kinahusika na mifumo yote inayotumika Hospitalini

Mifumo hiyo ni kama GOT HOMIS,GePG pamoja na intaneti

Kitengo cha ufuaji

kitengo hiki kinahusika na ufuaji wa shuka zinazotumiwa na wagonjwa.

Kitengo cha Afya na Mazingira

Kitengo hiki kina husika na Utunzaji wa mazingira ya Hospitali, matengenezo ya mfumo wa maji taka pamoja na usimamizi wa taka zinazozalishwa hospitalini.

Ustawi wa jamii

Kutoa ushauri na msaada wa kijamii, kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa unyanyasaji wa kijinsia 

Kutoa msmaha wa matibabu kwa wateja wasiojiweza