Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(Simiyurrh)

Mafunzo ya kusaidia Mtoto Kupumua

Posted on: March 19th, 2020

Chama cha wakunga tanzania tawi la mkoani simiyu (TAMA)

Leo tarehe 19 Machi 2020 Kimetoa mafunzo kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu juu ya kumsaidia Mtoto kupumua.

Mafunzo hayo yaliyowezeshwa na Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto kanda ya Ziwa  Neema Mshana  yamefanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu yakijumuisha jinsi ya kuleta tofauti kama mhudumu mwenye ujuzi na weledi.

Pia maandalizi ya mama kabla ya kujifungua,jinsi ya kumpatia joto mtoto na kukata kitovu, njisi ya kumpa mtoto pumzi kwa kutumia bag na mask vilifundishwa.

Aidha mafunzo haya yanalenga katika kupunguza vifo vya watoto wachanga